Raia mmoja wa Somalia ambaye anayedaiwa kuwa alikuwa mzungumzaji wa maharamia katika
kupokea vikomboleo kwa ajili maharamia wa Somalia walioteka nyara meli
moja ya Marekani mwaka uliopita na kuwauwa mateka wanne raia wa Marekani amehukumiwa vifungo 12 vya maisha na mahakama ya Marekani.
Mohamed Shibin alipatwa na hatia mwezi Aprili mwaka huu kwa makosa 15
yakiwemo uharamia, kuteka nyara na kula njama.
Mahakma hiyo ya Marekani imesema kuwa Shibin alilipwa kati ya dola elfu
30 hadi 50 kwa kazi yake ya kuwa mzungumzaji wa maharamia kwa ajili ya
kupatiwa kikomboleo.
CHANZO: REDIONYUMBANI
No comments:
Post a Comment