Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Marekani ina
nafasi haribifu kuhusiana na matukio ya Mashariki ya Kati.
Kuhusu
mpango wa Marekani wa kutaka kuanzisha eneo lisiloruhusiwa kupaa ndege
huko Syria, Ramin Mehmanparast Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
ameongeza kuwa Marekani imeazimia kufanya uharibifu na mauaji huko
Syria kama ilivyofanya huko Iraq, Afghanistan, Libya na katika nchi
nyinginezo.
Amesema Marekani inajaribu kila inaloweza kusababisha
mauaji mengi miongoni mwa raia na umma wa Kiislamu katika eneo la
Mashariki ya Kati. Ramin Mehmanparast amesema Marekani inafanya kila
iwezalo ili kunufaika zaidi sambamba na waitifaki wake.
Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema hivi sasa kunafanywa njama kwa
ajili ya kuandaa utangulizi wa kuzusha mapigano ya kijeshi huko Syria
kupitia kutangazwa eneo lisiloruhusiwa kupaa ndege na kwamba hiyo ni
tahadhari kwa nchi zote za eneo kwamba fitna kubwa inafanywa ili
kuzigombanisha nchi za Kiislamu katika eneo hili na kwamba Marekani na
Uzayuni zinafanya kila linalowezekana kwa malengo yao ya kisiasa
yakuzusha mapigano na kusababisha vifo vya raia wasio nan hatia na
kusababisha hasara kubwa katika eneo hili kwa maslahi ya utawala wa
Kizayuni.
No comments:
Post a Comment