MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame ametupilia mbali ombi lililotolewa na mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa la kutaka kusitishwa kwa utangazwaji wa matokeo ya urais na kutaka kazi hiyo ianze upya kwa madai kuwa maafisa wa usalama wa taifa wamechakachua matokeo hayo.