MARASHI

PLAN YOUR WORK AND WORK ON YOUR PLAN BUT, WHEN YOU FAIL TO PLAN, YOU PLAN TO FAIL

Monday, July 30, 2012

KIPOZI IN PRESS BRIEFING

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi akizungumza na wanahabari mara baada ya kuongoza mjadala kuhusu uzalishaji wa muhogo wilayani humo uliofanyika katika kijiji cha Zinga. Mjadala huu uliratibiwa na Shirika la Oxfam na kuwahusisha wakulima wanawake kama mpango endelevu wa kutambua na kuthamini mchango wa wakulima wanawake katika uzalishaji wa chakula.

WACHAGGA WAHITIMU PhD YA UBAGUZI: WAANZISHA, KUSHEREHEKEA CHAGGA DAY

Wachagga wakipata mbege katika tamasha la CHAGGA DAY lilofanyika katika  viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam jana na kushirikisha watu mbalimbali wa makabila ya kichaga.

Duh! hata waandishi wa habari kumbe walialikwa katika tamasha la Chagga Day namuona jamaa wa Press hapo.

KUFUTURU AU KUKUFURU? TANGU LINI MKRISTO KUFUTURU ILHALI HAJAFUNGA?

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja miongoni mwa Ma-Sista waliohudhuria katika ftari iliyoandaliwa na rais huyo ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.