MARASHI

PLAN YOUR WORK AND WORK ON YOUR PLAN BUT, WHEN YOU FAIL TO PLAN, YOU PLAN TO FAIL

Saturday, July 28, 2012

WAHITIMU MUM WASIRIKI SEMINA YA KUAGWA

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Waislaam Morogoro (MUM) akichangia mada iliyowasilishwa na Mhadhiri Msaidizi wa chuo hicho Suleiman Filambi. Picha na Ayoub Mvungi

Mhadhiri Msaidizi wa MUM Suleiman Filambi (katikati) akiteta jambo na Mhadhiri mwenzake wa chuo hicho Dk Athuman Mjinga (kushoto), aliyepo kulia ni mhadhiri msaidizi wa MUM katika Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Salim Said.

Mhadhiri Msaidi wa MUM katika kitengo cha Lugha Jaafar Siraj (katikati) akiwasilisha mada katika semina ya wahitimu wa chuo hico katika fani za Elimu, Maarifa ya Uislaam, Mawasiliano ya Umma n.k iliyofanyika katika Shule ya Kiislaam ya Darul-Arqam mkoani Morogoro.

Baadhi ya wahitimu wa MUM wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Sheikh Ponda Issa Ponda kuhusu Sensa na Katiba Mpya katika semina iliyofanyika hivi karibuni kwa ajili ya wahitimu hao mkoani Morogoro.

Baadhi ya wahitimu wakifuatilia mada.

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Jamal (kulia) na mwenzake wa MUM wakiwa katika semina ya wahitimu wa MUM hivi karibuni mkoani Morogoro.

Mhadhiri Msaidizi wa MUM Said Nassor Jaff akiwasilisha mada ya Umuhimu wa Ndoa katika semina ya wahitimu wa MUM hivi karibuni mkoani Morogoro.

Mhadhiri Msaidizi wa MUM Said Nassor Jaff (katikati) akiwasilisha mada, kulia ni Mhadhiri Msaidizi wa MUM Salim Said na kushoto ni mhadhiri wa MUM Dk Athuman Mjinga



Jaafar Siraj akichangia mada kulian ni mhadhir msaidizi wa MUM Khalid Liyeme



Baadhi ya wahitimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwao katika semina ya kuwaaga iliyofanyika hivi karibuni katika shule ya kiislaam ya Daarul-Arqam mkoani Morogoro. Picha zote na Ayoub Mvungi, MUM.