Baadhi ya wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya kina-mama Kata ya Mabibo jijini Dar es Salaam wakisheherekea kumaliza mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali yaliyofadhiliwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM katika Kata hiyo, Mlowe Boni na Mlezi wa Jumuiya hiyo Hawa Ng'umbi.
Tupo darasano tunasoma lakini vumbi linatusumbua. Hawa ni watoto wa moja ya shule za msingi katika wilaya ya Newala Mjini mkoa wa Mtwara.
HONGERA: Mkuu wa wilaya ya Newala Dk Rehema Nchinimbi, akitoa cheti kwa muhitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kitangari wilaya ya Newala mkoani Mtwara.
HATUSAFIRI:TUNAENDA KUFUA. Baadhi wa wanafunzi wa shule za msingi katika Wilaya ya Newala mkoani Mtwara wakiwa na mabegi yenye nguo chafu kwa ajili ya kwenda katika bonde la mto ruvuma kufua, takriban umbali wa Kilomita 7 kutoka wanakoishi.
TUPO KAZINI: Baadhi ya wapigapicha wakujitegemea wakihangaika kupata picha katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Kitangari wilaya ya Newala mkoani Mtwara
MGUU SAWA!: Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika paredi ya mchana katika moja ya shule za msingi za wilaya ya Newala mkoni Mtwara, ikiwa ni siku ya Jumanne. Hali ya usafi kwa wanafunzi hao ni mtihani kutokana na uhaba mkubwa wa maji unaoikabili wilaya hiyo