Waziri
wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akiongea na waandishi
wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwafukuza kazi
watumishi watatu wa wizara hiyo kutoka na ukiukaji wa sheria na
utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kufuatia sakata la usafirishaji wa
wanyama pori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwenda Quatar.
Wizara
ya Maliasili na Utalii imechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake
tisa (9) kufuatia kadhia ya utoroshaji wa Wanyamapori Hai katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine yanayohusu
Wanyamapori. Watumishi hao wamechukuliwa hatua husika kufuatia
kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.
(1) Waliofukuzwa kazi kutokana na ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ni:
-
Bw. Obeid F. Mbangwa - Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa
kadhia hiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Matumizi ya
Wanyamapori,
- Bw. Simon Charles Gwera – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,
- Bw Frank Mremi - Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.
(2)
Aliyeondolewa Cheo cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu
za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa
wanyama ni:
-
Bw. Bonaventura M.C. Midala – Mkurugenzi Msaidizi, Undelezaji
Wanyamapori. Wakati wa tukio alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya
Kuzuia Ujangili.
(3)
Wafuatao ni Maafisa Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo ya
Wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali la
Maandishi:
- Bibi Martha P. Msemo - Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.
- Bibi Anthonia Anthony – Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam.
(4)
Bw. Silvanus Atete Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii,
CITES na Utalii wa Picha Arusha aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo
ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka Sheria
katika utoaji wa vibali. Aidha, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu
taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.
- Silvanus Atete Okudo – amepewa Onyo Kali la Maandishi.
(5) Wafuatao ni Maafisa ambao uchunguzi dhidi yao unaendelea:
- Bw. Mohamed Madehele – Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori
- Bibi Mariam Nyallu – Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.
Wahusika
wengine katika kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili
na Utalii watachukiliwa hatua na mamlaka nyingine husika.
Mhe. Khamis Suedi Kagasheki
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII
13 Agosti 2012
Imetolewa kwenye Press Conference iliyofanyika Katika Viwanja vya Bunge Dodoma tarehe 13 Agosti 2012)
No comments:
Post a Comment