MABOMU YA MACHOZI YANAENDELEA KUPIGWA KIGAMBONI BAADA YA WACHIMBA KOKOTO KUFANYA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA
HALI
sasa si shwari eneo la Mji Mwema, Kigamboni, Dar es Salaam, baada ya
wachimba kokoto kufanya vurugu kwa kufunga barabara kwa mawe na kuwasha
matairi barabaran wakipinga kitendo cha Serikali kuwazuia kuchimba
kokoto.
Mkazi mmoja wa Mji Mwema aliye karibu na makazi ya Rais msitaafu wa wa Zanzibar Alhaji Aboud Jumbe, amesema hali ni mbaya kiasi cha asilimia kubwa ya wakazi wa eneo hilo kujifungia majumbani wakihofia vurugu hizo.
"Ndugu mwandishi wa habari, hali hivi sasa ni mbaya mno, mawasiliano ya usafiri yamekatika kwani wachimba kokoto waliozuiwa kufanya kazi yao, wameandamana huku wengine wakijaza kokoto na mawe barabarani na wengine wakichoma matairi, tunaogopa hivyo tumejifungia majumbani" alisema mama huyo.
Alisema mabomu ya machozi yanaendelea kupigwa na FFU ili kuwatawanya vijana hao, lakini inaelekea ni wabishi.
Blogu yako ya Kamanda wa Matukio itaendelea kuwapatia taarifa juu ya sakata hilo kwa kadri itakavyokuwa inazipata.

CHANZO: mwaikenda.blogspot.com
No comments:
Post a Comment