Baadhi ya waislaam na wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (Breweries) wakiwa katika pozi mbalimba waliposhiriki futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jana.
MARASHI
PLAN YOUR WORK AND WORK ON YOUR PLAN BUT, WHEN YOU FAIL TO PLAN, YOU PLAN TO FAIL
Friday, August 17, 2012
Thursday, August 16, 2012
MAREKANI YAENDELEZA MAUAJI SOMALIA
MOGADISHU
Ndege
za kigaidi zisizo na rubani za Marekani zimeendelea kufanya mauaji ya
watu katika nchi ya Waislamu ya Somalia iliyopo Afrika.
Watu
wasiopungua saba
wameauwa na wengine kumi
na saba
wamejeruhiwa katika mashambulizi ya jana Jumatano yaliyofanywa na
ndege hizo kwenye mji wa JOWHAR
nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.
Hadi
sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu hasara nyingine
zilizosababishwa na mashambulizi hayo ya kinyama.
Mbali
na nchini Somalia, Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizotumia rubani
kufanya mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Afghanistan, Pakistan,
Yemen na imewahi kutumia pia ndege hizo nchini Libya.
Marekani
inadai kuwa inashambulia wanamgambo wa AL-QAEDA
na AS-SHABBAB,
lakini wananchi wa kawaida ndio wahanga wakuu wa mashambulizi ya
ndege hizo za kigaidi.
MAELFU WAKIMBIA MAKAZI YAO
KINSHASA
MAPIGANO
ya miezi mitano sasa kati ya waasi wa kundi la M23
na Jeshi
la Jamhuri ya Kidemokrasia ya KONGO
yamewalazimisha zaidi ya watu nusu milioni kukimbia makazi yao huko
mashariki mwa nchi hiyo.
Ripoti
zinasema kuwa raia wengi wa maeneo ya Kivu
Kaskazini
yenye utajiri mkubwa wa madini wamelazimika kukimbia makazi yao baada
ya kujikuta katikati ya machafuko na mapigano ya kundi la M23
na Jeshi la serikali ya Kinshasa.
Maafa
hayo yanaendelea kuwapata raia wa kawaida wa KONGO
licha ya kuwepo maelfu ya askari wa Umoja wa Mataifa waliopelekwa
nchini humo kwa ajili ya kulinda amani.
Mamia
ya wakimbizi hao wa KONGO
wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani za RWANDA,
BURUNDI
na
UGANDA huku
Serikali ya KONGO
ikitoa shutuma kali kwa nchi ya RWANDA
na UGANDA kwa
kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23.
Waasi
wa M23
walijitenga na jeshi la serikali ya Kinshasa
wakidai kuwa serikali haijatekeleza vipengele vya makubaliano ya
amani yaliyotiwa saini MACHI
23, 2009.
HRW YAINGILIA KATI WAISLAAM KUKAMATWA ETHIPEA
ADDISABABA
Shirika
la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitaka
serikali ya Ethiopia kuwaachia huru viongozi 17 wa Kiislamu
waliokamatwa katika maandamano ya amani yaliyofanyika nchini humo.
Taarifa
iliyotolewa na hilo la Kutetea Haki za Binadamu imesema serikali ya
Ethiopia inapaswa kuwaachia huru viongozi hao 17 wa Kiislamu
waliotiwa nguvuni wakati askari wa usalama wa Ethiopea
walipowakandamiza kinyama wapinzani Waislamu mjini Addis Ababa.
Watu
hao walitiwa nguvuni katika maandamano makubwa ya amani yaliyofanywa
na Waislamu mwezi jana kupinga uingiliaji usio wa kisheria wa
serikali katika masuala ya Waislamu.
Shirika
la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesisitiza kuwa
mahabusu hao wanakabiliana na hali mbaya na wanashikiliwa bila ya
kujulishwa makosa yao au kuwa na wakili.
Waislamu
wanaunda zaidi ya asilimia 30 ya jamii ya watu milioni 83 ya
Ethiopia.
TRA WAPATA SCANNER MPYA TANGA
TANGA
MAMLAKA
ya Mapato Tanzania (TRA) Tawi la Tanga imepata mashine mpya ya
kisasa yenye uwezo wa kutambua bidhaa zilizohifadhiwa ndani ya
makontena (Scarner) na kuiwezesha mamlaka hiyo kufanya kazi zake kwa
ufanisi na haraka.
Meneja
wa Mamlaka hiyo Mkoani Tanga Nyonge Mahanyu, amesema mashine hiyo
itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wa mkoa huo kwa kuwa itaondosha
kero za wafanyabiashara kucheleweshewa shehena zao katika Bandari ya
Tanga.
Mahanyu
amesema awali wafanyabiashara wa Tanga walikuwa wakilalamikia
kucheleweshwa kwa ukaguzi wa mizigo yao bandarini hapo jambo
lililokuwa likitishia uhai wa bandari kongwe ya mkoa wa Tanga.
Amesema
baada ya ujio wa mashine hiyo utaweka mvuto kwa wafanyabiashara wengi
kwa kuwa wataweza kushusha shehena zao kwa wakati na bila ya
usumbufu.
Mahanyu
amefafanua kuwa mashine hiyo ina uwezo wa kukagua kontena moja kwa
dakika tatu tu jambo ambalo litaiwezesha TRA kukagua makontena mengi
ndani ya muda mfupi na hivyo kukusanya kodi nyingi tofauti na ilivyo
sasa.
Kwa
upande wake mtaalamu wa Scana Mhandisi Julias Joseph, amesema mashine
hiyo ambayo ina uwezo mkubwa wa kukagua na kutambua shehena zilizomo
ndani ya makontena itakuwa kimbilio la wafanyabiashara kushusha
bidhaa zao katika bandari ya Tanga.
Kutokuwapo
kwa ufanisi katika utoaji wa huduma katika Bandari ya mkoa wa Tanga
kumesababisha wafanyabiashara wengi nchini kuikimbia bandari hiyo na
kuamua kushushia mizigo yao katika bandari za Mombasa, Zanzibar na
Dar es Salaaa.
HATARINI 'KUTOGRADUATE'
ZANZIBAR
Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimesema wanafunzi wote
wanaomaliza masomo yao na ambao hawatakamilisha malipo ya ada hadi
Agosti 22 mwaka huu hawataruhusiwa kufanya mitihani yao ya muhula wa
pili kwa mwaka 2011/2012.
SUZA
inatarajia kuanza mitihani yake ya muhula wa pili ya kufunga mwaka
wasomo kuanzia Agosti 22 mwaka huu chuoni hapo.
Onyo
hilo limetolewa na Makamu Mkuu wa SUZA Professa Idriss Ahmad Rai
mbele ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kikao cha pamoja
kati ya uongozi wa chuo na serikali ya wanafunzi kwenye Makao Makuu
ya chuo hicho Vuga, mjini Unguja.
Profesa
Rai amesema onyo hilo halitawahusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa
pili ambao wameruhusiwa kufanya mitihani baada ya kujaza mkataba
maalum baina ya mwanafunzi binafsi na chuo.
Profesa
Rai amesema mkataba huo utawalazimisha wanafunzi hao kulipa
malimbikizo ya ada wanayodaiwa kabla ya kuanza muhula mpya wa masomo
unaotarajiwa kuanza Oktoba mwaka huu na kwamba watakaoshindwa kulipa
hawataruhusiwa kuanza masomo katika muhula huo.
Hata
hivyo amesema wanafunzi watakaoshindwa kuanza mitihani Agosti 22
mwaka watapewa nafasi ya kufanya mitihani wakati wa mitihani ya
marejeo (supplementary examination) lakini kwa upande wao utakuwa
ndio mtihani wa kawaida iwapo watakamilisha malipo ya madeni yao.
Professa
Rai amesema SUZA imeamua kufanya uwamuzi huo mzito kutokana na
wanafunzi wengi kushindwa kulipa ada zao na hivi sasa wanawadai kiasi
cha shilingi 270 milioni.
Amesema
lengo la chuo siyo kuwakomoa wanafunzi lakini ni njia ya kuhakikisha
wanapata fedha ambazo ni muhimu katika kukiendeleza chuo hicho pamoja
na ruzuku inayotolewa na Serikali.
Ameongeza
kuwa wanaelewa ugumu wa maisha unaowakabili wanafunzi wengi hasa
katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani na kuelekea sikukuu ya
IDD-EL-FITRI lakini alidai hakuna njia ya mkato ya kupata mapato ya
kuendesha chuo hicho.
NGALAWA AWAASA WAISLAAM
TANGA
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Chiku Ngallawa, amewataka Waislamu katika kipindi
hiki cha kuelekea mwisho wa mfungo wa Ramadhani kuhakikisha mafunzo
wanayoyapata kutoka kwa Mashekh wao wanayaendeleza hata baada ya
mfungo wa mwezi mtukufu.
Ngallawa
ameyasema hayo katika futari iliyoandaliwa na Bank ya CRDB tawi la
Tanga.
Ngallawa
amesema tabia ya upendo na kuoneana huruma katika jamii iliyojengeka
miongoni mwa waislaam kipindi hiki cha Ramadhani ni dalili za
kuyapokea mafunzo mbalimbali yanayotolewa na Masheikh.
Kwa
upande wake Meneja wa huduma kwa wateja wa CRDB Makao Makuu, Godwin
Semunyu, amesema kwa kuzingatia utukufu wa mwezi wa Ramadhani ndio
mana wamekuwa na utaratibu wa kufuturisha lengo likiwa ni kuleta
umoja na mshikamano katika jamii.
Semunyu
amesema CRDB itaendelea kuwa karibu na Waislamu hasa katika kipindi
cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kutoa misaada kadiri ya uwezo wake
kwa kuwkufanya hivyo ni faida kubwa kwa jamii na beki hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)



