ADDISABABA
Shirika
la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitaka
serikali ya Ethiopia kuwaachia huru viongozi 17 wa Kiislamu
waliokamatwa katika maandamano ya amani yaliyofanyika nchini humo.
Taarifa
iliyotolewa na hilo la Kutetea Haki za Binadamu imesema serikali ya
Ethiopia inapaswa kuwaachia huru viongozi hao 17 wa Kiislamu
waliotiwa nguvuni wakati askari wa usalama wa Ethiopea
walipowakandamiza kinyama wapinzani Waislamu mjini Addis Ababa.
Watu
hao walitiwa nguvuni katika maandamano makubwa ya amani yaliyofanywa
na Waislamu mwezi jana kupinga uingiliaji usio wa kisheria wa
serikali katika masuala ya Waislamu.
Shirika
la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesisitiza kuwa
mahabusu hao wanakabiliana na hali mbaya na wanashikiliwa bila ya
kujulishwa makosa yao au kuwa na wakili.
Waislamu
wanaunda zaidi ya asilimia 30 ya jamii ya watu milioni 83 ya
Ethiopia.
No comments:
Post a Comment