MAPIGANO
ya miezi mitano sasa kati ya waasi wa kundi la M23
na Jeshi
la Jamhuri ya Kidemokrasia ya KONGO
yamewalazimisha zaidi ya watu nusu milioni kukimbia makazi yao huko
mashariki mwa nchi hiyo.
Ripoti
zinasema kuwa raia wengi wa maeneo ya Kivu
Kaskazini
yenye utajiri mkubwa wa madini wamelazimika kukimbia makazi yao baada
ya kujikuta katikati ya machafuko na mapigano ya kundi la M23
na Jeshi la serikali ya Kinshasa.
Maafa
hayo yanaendelea kuwapata raia wa kawaida wa KONGO
licha ya kuwepo maelfu ya askari wa Umoja wa Mataifa waliopelekwa
nchini humo kwa ajili ya kulinda amani.
Mamia
ya wakimbizi hao wa KONGO
wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani za RWANDA,
BURUNDI
na
UGANDA huku
Serikali ya KONGO
ikitoa shutuma kali kwa nchi ya RWANDA
na UGANDA kwa
kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23.
Waasi
wa M23
walijitenga na jeshi la serikali ya Kinshasa
wakidai kuwa serikali haijatekeleza vipengele vya makubaliano ya
amani yaliyotiwa saini MACHI
23, 2009.
No comments:
Post a Comment