MOGADISHU
Ndege
za kigaidi zisizo na rubani za Marekani zimeendelea kufanya mauaji ya
watu katika nchi ya Waislamu ya Somalia iliyopo Afrika.
Watu
wasiopungua saba
wameauwa na wengine kumi
na saba
wamejeruhiwa katika mashambulizi ya jana Jumatano yaliyofanywa na
ndege hizo kwenye mji wa JOWHAR
nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.
Hadi
sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu hasara nyingine
zilizosababishwa na mashambulizi hayo ya kinyama.
Mbali
na nchini Somalia, Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizotumia rubani
kufanya mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Afghanistan, Pakistan,
Yemen na imewahi kutumia pia ndege hizo nchini Libya.
Marekani
inadai kuwa inashambulia wanamgambo wa AL-QAEDA
na AS-SHABBAB,
lakini wananchi wa kawaida ndio wahanga wakuu wa mashambulizi ya
ndege hizo za kigaidi.
No comments:
Post a Comment