MARASHI
PLAN YOUR WORK AND WORK ON YOUR PLAN BUT, WHEN YOU FAIL TO PLAN, YOU PLAN TO FAIL
Sunday, August 19, 2012
SWALA YA IDD KITAIFA RUVUMA
Muft wa Tanzania Issa bin Shaaban Simba akiwa katika pozi mbalimbali aliokuwa akihudhuria swala ya IDD iliyoswaliwa kitaifa Mkoani Ruvuma.
SWALA YA IDD MASJID BAKWATA MAKAO MAKUU
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika pozi mbalimbali alipokwenda kuswali swala ya Idd katika viwanja vya Bakwata Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
SWALA YA IDD MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais Dk Moh'd Gharib Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi wakiwa katika pozi mbalimbali wakati na baada ya kuswali Idd katika Viwanja vya Mnazi Mmmoja jijini Dar es Salaam.
Friday, August 17, 2012
BREWERIES YAFUTARISHA: NI UPI UHALALI WA FUTARI HIYO, NINI HUKUMU YA MUISLAM ALIYEKUBALI KUFUTARISHWA NA KAMPUNI YA POMBE?
Baadhi ya waislaam na wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (Breweries) wakiwa katika pozi mbalimba waliposhiriki futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jana.
Thursday, August 16, 2012
MAREKANI YAENDELEZA MAUAJI SOMALIA
MOGADISHU
Ndege
za kigaidi zisizo na rubani za Marekani zimeendelea kufanya mauaji ya
watu katika nchi ya Waislamu ya Somalia iliyopo Afrika.
Watu
wasiopungua saba
wameauwa na wengine kumi
na saba
wamejeruhiwa katika mashambulizi ya jana Jumatano yaliyofanywa na
ndege hizo kwenye mji wa JOWHAR
nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.
Hadi
sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu hasara nyingine
zilizosababishwa na mashambulizi hayo ya kinyama.
Mbali
na nchini Somalia, Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizotumia rubani
kufanya mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Afghanistan, Pakistan,
Yemen na imewahi kutumia pia ndege hizo nchini Libya.
Marekani
inadai kuwa inashambulia wanamgambo wa AL-QAEDA
na AS-SHABBAB,
lakini wananchi wa kawaida ndio wahanga wakuu wa mashambulizi ya
ndege hizo za kigaidi.
MAELFU WAKIMBIA MAKAZI YAO
KINSHASA
MAPIGANO
ya miezi mitano sasa kati ya waasi wa kundi la M23
na Jeshi
la Jamhuri ya Kidemokrasia ya KONGO
yamewalazimisha zaidi ya watu nusu milioni kukimbia makazi yao huko
mashariki mwa nchi hiyo.
Ripoti
zinasema kuwa raia wengi wa maeneo ya Kivu
Kaskazini
yenye utajiri mkubwa wa madini wamelazimika kukimbia makazi yao baada
ya kujikuta katikati ya machafuko na mapigano ya kundi la M23
na Jeshi la serikali ya Kinshasa.
Maafa
hayo yanaendelea kuwapata raia wa kawaida wa KONGO
licha ya kuwepo maelfu ya askari wa Umoja wa Mataifa waliopelekwa
nchini humo kwa ajili ya kulinda amani.
Mamia
ya wakimbizi hao wa KONGO
wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani za RWANDA,
BURUNDI
na
UGANDA huku
Serikali ya KONGO
ikitoa shutuma kali kwa nchi ya RWANDA
na UGANDA kwa
kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23.
Waasi
wa M23
walijitenga na jeshi la serikali ya Kinshasa
wakidai kuwa serikali haijatekeleza vipengele vya makubaliano ya
amani yaliyotiwa saini MACHI
23, 2009.
HRW YAINGILIA KATI WAISLAAM KUKAMATWA ETHIPEA
ADDISABABA
Shirika
la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitaka
serikali ya Ethiopia kuwaachia huru viongozi 17 wa Kiislamu
waliokamatwa katika maandamano ya amani yaliyofanyika nchini humo.
Taarifa
iliyotolewa na hilo la Kutetea Haki za Binadamu imesema serikali ya
Ethiopia inapaswa kuwaachia huru viongozi hao 17 wa Kiislamu
waliotiwa nguvuni wakati askari wa usalama wa Ethiopea
walipowakandamiza kinyama wapinzani Waislamu mjini Addis Ababa.
Watu
hao walitiwa nguvuni katika maandamano makubwa ya amani yaliyofanywa
na Waislamu mwezi jana kupinga uingiliaji usio wa kisheria wa
serikali katika masuala ya Waislamu.
Shirika
la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesisitiza kuwa
mahabusu hao wanakabiliana na hali mbaya na wanashikiliwa bila ya
kujulishwa makosa yao au kuwa na wakili.
Waislamu
wanaunda zaidi ya asilimia 30 ya jamii ya watu milioni 83 ya
Ethiopia.
Subscribe to:
Posts (Atom)