Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali,
alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba akiwa katika
ziara maalum ya Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba.
MARASHI
PLAN YOUR WORK AND WORK ON YOUR PLAN BUT, WHEN YOU FAIL TO PLAN, YOU PLAN TO FAIL
Tuesday, July 31, 2012
JK ASHIRIKI MAZISHI YA SHEMEJIYE HUKO LINDI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika mazishi ya shemeji yake, Marehemu
Amani Kinyozi, katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi. PICHA NA IKULU.
ZAZIBAR 'KUSHNEI': VIONGOZI WAISALITI NCHI, ROHO ZA WAZANZIBAR ZAFANYIWA PUBLICTY KAMPUNI ZA POMBE
Makamu
wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally
Iddy akipeana mkono na Makau wa rais wa ZFA, Kassum Suleman.
Meneja Masoko wa Kinywaji cha Grandmalt, Fimbo Buttalah (kulia)
akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi mfano wa Hundi yenye thamani ya Shilingi
milioni tano kama sehemu ya Rambirambi zilizotolewa kwa pamoja kati ya
Grandmalt ambao ni wadhamini wa Ligi kuu ya Zanzibar.
Monday, July 30, 2012
KIPOZI IN PRESS BRIEFING
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi akizungumza na wanahabari mara baada ya kuongoza mjadala kuhusu uzalishaji wa muhogo wilayani humo uliofanyika katika kijiji cha Zinga. Mjadala huu uliratibiwa na Shirika la Oxfam na kuwahusisha wakulima
wanawake kama mpango endelevu wa kutambua na kuthamini mchango wa wakulima
wanawake katika uzalishaji wa chakula.
WACHAGGA WAHITIMU PhD YA UBAGUZI: WAANZISHA, KUSHEREHEKEA CHAGGA DAY
Wachagga wakipata mbege katika tamasha la CHAGGA DAY lilofanyika katika viwanja
vya
Leaders jijini Dar es salaam jana na kushirikisha watu mbalimbali wa
makabila ya kichaga.
Duh! hata waandishi wa habari kumbe walialikwa katika tamasha la Chagga Day namuona jamaa wa Press hapo.
KUFUTURU AU KUKUFURU? TANGU LINI MKRISTO KUFUTURU ILHALI HAJAFUNGA?
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja miongoni mwa Ma-Sista waliohudhuria katika ftari iliyoandaliwa na rais huyo ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.
Saturday, July 28, 2012
WAHITIMU MUM WASIRIKI SEMINA YA KUAGWA
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Waislaam Morogoro (MUM) akichangia mada iliyowasilishwa na Mhadhiri Msaidizi wa chuo hicho Suleiman Filambi. Picha na Ayoub Mvungi |
Baadhi ya wahitimu wakifuatilia mada. |
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Jamal (kulia) na mwenzake wa MUM wakiwa katika semina ya wahitimu wa MUM hivi karibuni mkoani Morogoro. |
Mhadhiri Msaidizi wa MUM Said Nassor Jaff akiwasilisha mada ya Umuhimu wa Ndoa katika semina ya wahitimu wa MUM hivi karibuni mkoani Morogoro. |
Mhadhiri Msaidizi wa MUM Said Nassor Jaff (katikati) akiwasilisha mada, kulia ni Mhadhiri Msaidizi wa MUM Salim Said na kushoto ni mhadhiri wa MUM Dk Athuman Mjinga |
Jaafar Siraj akichangia mada kulian ni mhadhir msaidizi wa MUM Khalid Liyeme |
Friday, July 27, 2012
WATEMBEA NUSU UCHI, MAKOBE MARUFUKU ZNZ
Khamis Amani, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imepiga marufuku mambo mbali mbali yanayoenda kinyume na maadili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikiwemo uvaaji wa nguo zisizokuwa na heshima, ili kulinda heshima ya mwezi huo.
Pamoja na marufuku hiyo, serikali imetanabahisha kuwa hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaokiuka agizo hilo la
serikali.
Mawaziri wa wizara za Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary, pamoja
na waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk,
waliyasema hayo katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani walipozungumza na
waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali.
Katika taarifa hiyo, Mawaziri hao walisema katika kipindi cha nyuma
mwezi mtukufu wa Ramadhani umekuwa ukipoteza heshima yake, kutokana na
waumini wake kuwa mstari wa mbele kuudharau mwezi huo.
“Tumezowea kuona watu wanakula ovyo, wanapiga disko mchana, uvaaji wa
nguo zisizokuwa na heshima kwa wanawake pamoja na mambo mengine, ambayo
yanaupotezea heshima mwezi huo mtukufu wa Ramadhani”, alisema waziri wa
Katiba na Sheria.
Hivyo waziri Abubakar alisema kwa kuona hayo serikali imeona ipo haja
ya kuendeleza tabia na hulka ya kuheshimu mwezi huo, kwa kupiga
marufuku mambo yote yanayokwenda kinyume na mila, silka na maadili ya
mwezi huo wa Ramadhani.
Katika marufuku hiyo, waziri Abubakar amepiga maruku kuwepo kwa
magenge ya vyakula (mama ntilie) na hoteli ndogo ndogo za kawaida kwa
mchana wote wa mwezi mtuku wa Ramadhani.
Waziri Abubakar alisema Serikali, haitoruhusu mtu yoyote wakati wa
mchana wa mwezi wa Ramadhani hata kwa yule asiyekuwa muumini wa dini ya
Kiisilamu, kuonekana akila, akinywa au akilewa hadharani, au kufanya
jambo lolote ambalo ni kinyume na maadili na silka za Zanzibar.
Pamoja na marufuku hiyo amepiga marufuku kwa mtu yoyote kwa wakati
wote kuvaa nguo zisizokuwa za heshima na zinazoonesha maumbile yake ya
siri, au nguo zinazobana ili kumfanya binaadamu mwengine kuwa na hisia
tofauti.
Sambamba na hayo, pia amepiga marufuku ‘disko toto’ kwa wakati wowote
ule, kwa madhumuni ya kuwafundisha watoto maadili mazuri ya Kizanzibari
na siyo kuiga mambo yasiyo na tija kwa vijana ambao ndio wazee na
viongozi wa taifa hili hapo baadae.
Alifahamisha kuwa, katika kipindi hicho cha sikukuu watoto wadogo
hawataruhusiwa kwenda katika sherehe baada ya saa 12 za jioni, hatua
kali za kisheria zitachukuliwa kwa mzee wa mtoto atakaekamatwa akikiuka
utaratibu huo.
“Tunaviomba vyombo vya dola na Baraza la Manispaa kuwachukulia hatua
za kisheria wale wote wanaohusika”, alisisitiza Waziri huyo wa Katiba na
Sheria.
Kwa upande wake, waziri wa Habari, Utamauni, Utalii na Michezo Said
Ali Mbarouk amesema kuwa, msimu wa utalii mwaka huu umeingia katika
mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivyo jukumu la wadau wote
wanaujishughulisha na biashara hiyo pamoja na wananchi kwa ujumla
kuwakumbusha na kuwaelekeza wageni kujiepusha kabisa na mambo yote
ambayo hayaruhusiwi kufanywa wakati wanaofunga wakiwa katika ibada hiyo.
“Tuwakumbushe wageni wetu mambo yasiyostahiki kwa mfano kula, kunywa,
kuvuta sigara na kubusiana hadharani ni mambo ambayo hayaruhusiwi na
yanakwenda kinyume na mila, silka na maadili yetu”, alisema Waziri
Mbarouk.
Alisema kuwa hali hiyo, itasaidia kuwaepusha na matendo yoyote
yanayoweza kuleta na kusababisha waliofunga kutokubali kufanywa kwa
vitendo hivyo hadharani, na hivyo kuwa chanzo cha vurugu baina ya
waumini wa Kiisilamu na wafuasi wengine.
Alisihi kuwa, ikitokezea kwa mgeni kwenda kinyume na hayo, jamii
iepuke matumizi ya nguvu katika kurekebisha hali hiyo na badala yake
itumike busara zaidi, na kuwafahamisha wageni nini cha kufanya na maeneo
gani wanaweza kupata huduma za lazima bila ya kuvunja sheria.
Alifahamisha kuwa, kikawaida watalii ni wageni wenye uwerevu,
usikivu, utiifu na wepesi wa kufuata maelekezo ya wenyeji wao, kwa
kuzingatia hayo kila mmoja ana wajibu wa kushirikiana nao.
Alisema wizara kupitia Kamisheni ya Utalii, tayari imeshasambaza
toleo ‘circular’ maalumu katika taasisi zote zinazohusika na utalii, kwa
nia na madhumuni ya kuendeleza utalii uwe endelevu.
MUM YAPOTEZA 14 AJALI YA MV SKAGIT
CHUO Kikuu cha Waislamu kilichoko mkoani Morogoro kimepoteza wanafunzi
14 wa mwaka wa kwanza katika ajali ya boti ya Mv Skagit iliyotokea Julai
18, mwaka huu katika Bahari ya Hindi karibu na kisiwa cha Chumbe.
Waliofariki na sehemu wnazotoka katika mabano ni Abdalla Mohamed wa
Unguja; Suleimani Ally (Pemba); Othumani Mwinyi Hussein (Unguja);
Rashid Salehe (Unguja); na Rashidi Juma (Pemba).
Wengine ni Hussan Seif (Unguja); Mangi Haji (Unguja); Asha Abdalla (Pemba); Said Iddi (Unguja); Khadija Khamis (Pemba); Mgeni Omari (Unguja); Patima Simai (Unguja); Said Khatib (Pemba) na Khamis Suleimani (Unguja).
Wengine ni Hussan Seif (Unguja); Mangi Haji (Unguja); Asha Abdalla (Pemba); Said Iddi (Unguja); Khadija Khamis (Pemba); Mgeni Omari (Unguja); Patima Simai (Unguja); Said Khatib (Pemba) na Khamis Suleimani (Unguja).
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari wa chuo
hicho, Saddy Ally, ilisema miili ya wanafunzi 12 ilipatikana na kuzikwa
na miwili haijapatikana.
Alisema kuwa msiba huo ni mkubwa na pigo kubwa kwa chuo hicho na kwa Taifa kwa ujumla.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Hamza Njozi, aliwapa pole wale wote
waliofikwa na msiba huo na kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza
ndugu zao katika ajali hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki
kigumu.
Aidha, Profesa Njozi alisema ni jambo la kusikitisha sana kwani chuo
kimepoteza wanafunzi wengi ambao walikuwa ni wa mwaka wa kwanza licha ya
kwamba pia katika ajali ya Mv Spice iliyotokea mwaka jana wanafunzi
wawili wa chuo hicho waliopoteza maisha.
HAMAD MASOUD AWAJIBIKA KISIASA
Salma Said, Zanzibar
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud
Hamad amejiuzulu wadhifa wake leo jioni imeelezwa.
Kwa mujibu wa
taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk.
Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la
Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.
“Tarehe 20 Julai,2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano
Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohammed Shein ya
kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit
iliyotokea Julai 18,2012” Ilisema taarifa ya Dk. Mzee.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dk Shein amemteua Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani(CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.
“Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,Rais amemteua Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano” Taarifa ya Ikulu ilisema.
Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano umeanza Julai 23 mwaka huu.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit.
Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni Meja Jenerali S.S. Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dk Shein amemteua Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani(CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.
“Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,Rais amemteua Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano” Taarifa ya Ikulu ilisema.
Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano umeanza Julai 23 mwaka huu.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit.
Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni Meja Jenerali S.S. Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.
WAZANZIBAR WAMECHOKA KUTUMIWA ROHO ZAO KUWA CHOMBO CHA PUBLICITY
Imefika wakati Shein na Balozi Seif Idd waone aibu kutokea mbele ya kamera za wanahabari kupokea rambirambi ambazo lengo lake kubwa ni watu, makampuni, taasisi na asasi za serikali kujitafutia umaarufu kupitia vifo vya watu.
Swali la kujiuliza kwa nini hao wanaojiita wasamaria wema hawataki kukabidhi misaada au rambirambi zao bila ya kuwapo kwa kamera za wanahabari au kukabidhi kwa viongozi wa ngazi za chini katika nchi.
Kila siku lazima wampate rais au makamu wa rais hata waziri, naibu, katibu mkuu na mkurugenzi wa wizara husika hawawataki.
Ni vyema Shein na Seif Idd wakakumbuka kuwa fedha wanazopokea zina damu kwani hazina nia nzuri ya kusaidia na wazanzibari wamechoka na tabia ya kutumiwa roho za ndugu na jamaa zao kama daraja la wafanyabiashara na wanasiasa kujipatia umaarufu.
Tafakarini halafu muchukue hatua.
SMZ YATILIA 'VIRINGI NGU ZA KUAZIMA', YATANGAZA BAKHERESA ATALETA MELI, BADALA YA KUWAELEZA WANANCHI NINI ITAFANYA KUMALIZA ADHA YA USAFIRI
Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati
ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na
meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo.
Aidha
meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha
zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa
dhidi ya wamiliki wa Meli hizo.
Kauli hiyo imetolewa na
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein
Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake
kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar.
Amesema
Mamlaka hiyo imefanya tathmini na uhakiki wa kutosha na kujiridhisha
kuwa Meli hizo hazifai kufanya kazi katika maeneo ya Zanzibar jambo
ambalo limepelekea kuchukua hatua za kufuta hati za kufanyia kazi meli
hizo.
Amefahamisha kuwa sababu kuu zilizopelekea Mamlaka
kufanya maamuzi hayo ni pamoja na uchakavu,umri wa meli hizo kuwa mrefu
na kupata matatizo mara kwa mara katika safari zao.
Kombo amefahamisha
kuwa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri na Bandari Zanzibar ya mwaka 2006
kifungu cha 17.1 inampa mamlaka Msajili wa Meli kuifuta meli yoyote
ambayo itakuwa haikidhi usalama wa abiria.
Kufuatia sheria
hiyo Kombo amesema watawataka wamiliki wa Meli hizo kuzirudisha hati za
kufanyia kazi meli hizo ili waende kutafuta sehemu nyengine za usajili
kinyume na maeneo ya Zanzibar.
Akizungumzia Meli ya
Mv.Serengeti Kombo amesema wamelazimika kuiagiza meli hiyo kupunguza
idadi ya abiria kutoka watu 800 hadi 350 na tani za mizigo kutoka 100
hadi 50 hadi pale ambapo watajiridhisha kutokana na hali ya meli hiyo
ilivyo.
Aidha amegusia kuwa Kampuni ya Bakhresa italeta
Meli kubwa ya abiria itakayofanya kazi zake Zanzibar ambapo pia Serikali
ya Mapinduzi nayo iko mbioni kuhakikisha wanaleta meli inayokidhi
mahitaji ya wananchi wa Zanzibar.
Subscribe to:
Posts (Atom)