MARASHI

PLAN YOUR WORK AND WORK ON YOUR PLAN BUT, WHEN YOU FAIL TO PLAN, YOU PLAN TO FAIL

Tuesday, June 2, 2009

Bonyokwa walia na barabara

Bonyokwa walilia barabara

Salim Said
CHAMA cha Madereva na Makondakta wa daladala zinazotoa huduma za usafiri kati ya Bonyokwa na Kimara Mwisho, kimeiomba serikali kukarabati barabara inayotumiwa magari hayo, ili kuepushia adha wananchi.

Chama hicho kimesema hali ya barabara hiyo ni mbaya na haipitiki kwa urahisi.

Wakizungumza na Mwananchi katika ofisi za chama hicho jana, baadhi ya viongozi walisema barabara inayounganisha Bunyokwa na Kimara Miwsho, imeharibiwa na mvua zilizomalizika hivi karibuni.

Mwenyekiti wa chama hicho, Shaaban Yussuf, alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha magari kuharibika na hivyo kuwa kero kwa wananchi.

“Njia hii ina abiria wingi lakini utakuta gari ni chache, kwa sababu matajiri hawataki kupeleka gari zao kwa sababu ya ubovu wa barabara,” alisema Yussuf.

Alisema kwa kuzingatia umuhimu wa barabara hiyo, kuna haja kwa mamlaka zinazohusika kuifanyia matengenezo ya haraka.

Shaban pia alikanusha madai kuwa chama hicho kimekuwa kikikusanya fedha kwa ajili matengenezo ya barabara hiyo.

“Madai hayo hayana ukweli, nadhani yakuzwa na watu wanaotaka kuwania uongozi katika serikali za mitaa,” alinena.

Kwa upande wake, Katibu wa chama hicho, Peter Mbuya, alisema wao kama wadau, wameamua kurekebisha baadhi ya maeneo korofi katika barabara hiyo, ili kurahisisha usafiri kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment