MARASHI

PLAN YOUR WORK AND WORK ON YOUR PLAN BUT, WHEN YOU FAIL TO PLAN, YOU PLAN TO FAIL

Saturday, June 26, 2010

USIWE NA WASIWASI UTASHINDA


Waziri Haroun akisalimiana na baadhi ya wazee wa CCM Zanzibar katika ofisi za chama hicho Kisiwandui mjini Unguja muda mfupi kabla ya kuchukua fomu ya kugombea uraisi wa Zanzibar. Picha na Salim Said.

KARIBU BABA


Waziri Haroun akiingia katika ukumbi wa hoteli ya Tembo Malindi mjini Unguja kwa ajili kukutana na wanahabari muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea uraisi wa zanzibar. Picha na Salim Said.




Waziri Haroun katika matukio mbalimbali siku ya kuchukua fomu ya kuwania uraisi wa Zanzibar. Mwenye shati jeusi ni mtoto wake. Picha zote na Salim Said.

DUA KWA MZEE





Picha mbalimbali zikimuonyesha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Haroun Ali Suleiman naa baadhi ya wana-CCM katika kaburi la raisi wa kwanza wa Zanzibar hayati, Abeid Amani Karume kuomba dua muda mfupi kabla ya kuchukua fomu ya kugombea uraisi wa Zanzibar juzi mjini Unguja. Picha zote na Salim Said.

KUSALIMIA MZEE KARUME KWANZA


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Haroun Ali Suleiman na msafara wake akielekea katika kaburi la Raisi wa kwanza wa visiwasiwa hivyo, Hayati Mzee Abeid Amani Karume kuomba dua na baadaye kwenda kuchukua fomu ya kutafuta ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kugombea uraisi wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa 2010. Picha na Salim Said