Salim Said
SERIKALI imekiri kulemewa na shehena ya tani zaidi ya 290 za samaki zilizokamatwa kwenye meli ya MV Tawariq 1 iliyokuwa ikifanya uvuvi haramu kwenye pwani ya Tanzania.
Imedaiwa kuwa samaki hao wanahifadhiwa kwa gharama ya Dola 80 za Marekani kwa tani moja kila siku na kampuni Bahari Foods Limited ya Dar es Salaam kuanzia Machi 8 mwaka huu.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli alisema juzi Dar es Salaam kuwa, gharama hizo ni mzigo kwa serikali ambayo hadi sasa haijui hatima yake.
“Ni kweli serikali inaendelea kuumia,” alisema Magufuli bila kutaja kiwango cha gharama inayolipia shehena hiyo lakini akibainisha kuwa suala hilo lipo chini ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
“Serikali inaheshimu mahakama na wala haiwezi kuingilia kazi yake, kwa hiyo mahakama ndio itakayoamua hatma ya samaki hao,” alisema Magufuli
Alieleza kushangazwa kwake na jinsi kesi hiyo inavyocheleweshwa akitolea mfano wa mahakama katika nchi zingine za Afrika ikiwamo Namibia ambako alisema kuwa hukumu za kesi za aina hiyo hazichukui siku tano
No comments:
Post a Comment